Sunday, January 31, 2016

EMIRATES FA CUP DROO RAUNDI YA 5 KUFANYIKA LEO!

Katika Mechi ya mwisho ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP iliyochezwa Jana huko Anfield, Liverpool ilibanwa na West Ham na kutoka 0-0.
Timu hizi sasa zitarudiana huko Upton Park Mwezi Februari na Mshindi kusonga Raundi ya 5 ya Kombe hili ambayo Drro yake itafanyika baadae Leo.
Hii ni mara ya 3 kwa Liverpool na West Ham kukutana Msimu huu na katika mara 2 za kwanza, West Ham waliichapa Liverpool 3-0 huko Anfield na 2-0 huko Upton Park katika Mechi za Ligi Kuu England.
Leo Jumapili ziko Mechi mbili tu za Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP kati ya Carlisle na Everton na kisha MK Dons na Mabingwa wa England Chelsea..

DROO ya Raundi ya 5 ya FA CUP:
-Namba za Timu kwenye Chungu cha Droo ambapo Timu yeyote inaweza kuibuka kucheza na yeyote

-Mechi kuchezwa Wikiendi ya Februari 19 hadi 20.

1 West Bromwich Albion au Peterborough Unite2
2 Leeds United
3 Arsenal
4 Manchester United
5 Reading
6 Liverpool au West Ham United
7 Manchester City
8 Shrewsbury Town
9 Watford
10 Carlisle United au Everton
11 Crystal Palace
12 Blackburn Rovers
13 AFC Bournemouth
14 Tottenham Hotspur
15 Hull City
16 MK Dons au Chelsea

EMIRATES FA CUP
Raundi ya 4
Ratiba

Jumapili Januari 31
16:30 Carlisle v Everton
19:00 MK Dons v Chelsea

THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016

Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016