Thursday, January 21, 2016

EMIRATES FA CUP: MARUDIO RAUNDI YA 3, LIVERPOOL YAMPIGA EXETER 3-0, SPURS 2-0 LEICESTER

JANA, kwenye Mechi za Marudiano za Raundi ya 3 ya EMIRATES FA CUP, Liverpool na Tottenham zilifanikiwa kushinda na kutinga Raundi ya 4.
Huko King Power Stadium, ikiwa ni Marudiano baada ya Sare ya 2-2 kwenye Mechi iliyochezwa White Hart Lane, Tottenham walilipiza kisasi cha Wikiendi iliyopita cha kufungwa 1-0 na Leicester City kwa kuwachapa Vinara hao wa Ligi Kuu England Bao 2-0.
Bao za Spurs azilifungwa na Son Heung-min, Dakika ya 39, na Nacer Chadli, Dakika ya 66.
Kwenye Raundi ya 4, Tottenham watacheza Ugenini na Timu ya Daraja la chini, Colchester.
Huko A,nfield, baada ya kutoka Sare 2-2 huko Exeter City na Timu ya Daraja la chini, Exter, Jana Liverpool waliwanyuka wanyonge hao Bao 3-0.

Bao za Liverpool zilifungwa na Joe Allen, Dakika ya 10, Oluwaseyi Ojo, Dakika ya 74 na Joao Carlos, Dakika ya 82.
Kwenye Raundi ya 4, Liverpool watakuwa kwao Anfield kucheza na wenzao wa Ligi Kuu England West Ham.

EMIRATES FA CUP
Raundi ya 4
Ijumaa Januari 29

2255 Derby v Man United
Jumamosi Juni 30
1545 Colchester v Tottenham  

Zote kuanza Saa 12 Jioni
Arsenal v Burnley
Crystal Palace v Stoke
Nottm Forest v Watford
Oxford Utd v Blackburn
Shrewsbury v Sheff Wed
Portsmouth v Bournemouth
Aston Villa v Man City


Reading v Walsall
Bolton v Leeds
West Brom v Peterborough
Bury v Hull
2030 Liverpool v West Ham
Jumapili 31 January 2016
1630 Carlisle v Everton
1900 MK Dons v Chelsea
 

THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016