Sunday, January 10, 2016

FA CUP: TOTTENHAM HOTSPURS 2 v 2 LEICESTER CITY, PENATI YA DAKIKA YA MAJERUHI YA KANE YAOKOA JAHAZI KWA SPURS!


Kane akifanya yake kwenye mkwaju wa penati
PENATI  ya Dakika ya 89 iliyofungwa na Harry Kane imewaokoa Tottenham walipokuwa kwao White Hart Lane na kuwapa Sare ya 2-2 na Leicester City kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya EMIRATES FA CUP.
Timu hizi sasa zitarudiana huko King Power Stadium kwenye Tarehe itakayothibitishwa baadae.
Tottenham walitangulia kufunga katika Dakika ya 8 kwa Bao la Christian Eriksen na Leicester kusawazisha Dakika ya 19 kwa Kichwa cha Marcin Wasilewski.
Kipindi cha Pili, Mchezaji alietoka Benchi, Shinji Okazaki, Dakika ya 48, akawapa Leicester Bao la Pili na kuongoza 2-1.
Ndipo ikaja Dakika ya 89 na Harry Kane, alieanzia Benchi, kuwapa Bao la kusawazisha kwa Penati iliyotolewa ya Refa kudai Nathan Dyer aliunawa Mpira.

Shinji Okazaki, Dakika ya 48, akawapa Leicester Bao la Pili na kuongoza 2-1.