Friday, January 8, 2016

FA CUP: OLD TRAFFORD JUMAMOSI MANCHESTER UNITED V SHEFFIELD UNITED.

BAADA ya kuanza poa 2016 kwa kuitwanga Swansea City 2-1 kwenye Ligi Kuu England, sasa Manchester United wako tena kwao Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP na Sheffield United inayocheza Daraja la chini, Ligi 1,ikiwa ni Madaraja Mawili chini ya Ligi Kuu England.
Man United wanaanza kampeni ya kulitwaa Kombe hili ambalo mara ya mwisho walilichukua Mwaka 2004, ikiwa ni mara yao ya 11, na wamepitwa tu na Arsenal waliolitwaa mara 12 baada ya kulibeba mara 2 mfululizo kwa Miaka Miwili iliyopita.

Wakati Man United wakitoka kwenye ushindi kuelekea Mechi hii, Sheffield United wao wanatoka kwenye kipigo cha 3-2 toka kwa Peterborough katika Mechi ya Ligi 1 kilichomaliza ushindi wao wa Mechi 4 mfululizo na kuwatupa Nafasi ya 8.
Sheffield United wapo Raundi hii ya 3 ya FA CUP baada ya kuanza Raundi mbili nyma kwa kuzitoa Timu ambayo haiku kwenye mfumo wa Ligi Worcester City 3-0 na Timu ya Ligi 1, Oldham Athletic 1-0.

Man United, kama zilivyo Timu nyingine za Ligi Kuu England na Daraja la Championship, zinaanzia Raundi hii.
 

Hali za Wachezaji
Ukiwaondoa Majeruhi wa muda mrefu Marcos Rojo, Antonio Valencia na Luke Shaw, Man United watamkosa pia Phil Jones alieumia kwenye Mechi yao iliyopita na Swansea lakini Straika Chipukizi Jesse Lingard amepona na anaweza kucheza Mechi hii. Sheffield hawana matatizo na Meneja wao Nigel Adkins anaweza pia kumrejesha Kikosini Kiungo Matt Done ambae hakucheza walipofungwa na Peterborough.