Friday, January 8, 2016

FA CUP: EXETER CITY 2 vs 2 LIVERPOOL


Dakika 90 zimekamilika mtanange ukimalizzika kwa sare ya 2-2.
KLABU ya Ligi 2, Exeter City Jana nusura iitwange Liverpool katika Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini, ilipotoka Sare ya 2-2 huko Mjini Exeter.
Exeter walitangulia kufunga kwa Bao la Tom Nichols na Liverpool, waliochezesha Kikosi kilichobadilika, walisawazisha kwa Goli la Jerome Sinclair.
Lee Holmes akaipa Exeter Bao la Pili na Liverpool kurudisha zikisalia Dakika 17 Mpira kwisha kwa Goli la Brad Smith.
Timu hizi zitarudiana huko Anfield katika Tarehe itayopangwa baadae na Marudiano hayo yatawanufaisha sana Exter, Timu ya Daraja la chini, kwa kuwapa Mapato yanayokadiriwa kufikia Pauni 700,000.

Smith dakika ya 73 aliwasawazishia bao Liverpool kwa kufanya 2-2Exeter City bao lao limefungwa na Tom Nicholls mapema dakika ya 9 huku Liverpool wakisawazisha kupitia kwa Jerome Sinclair dakika ya 12 na kufanya 1-1.Klopp