Monday, January 11, 2016

FIFA Ballon d'Or - NANI BORA DUNIANI, RONALDO, MESSI AU NEYMAR? LEO KUJULIKANA.

MESSI, RONALDO NA NEYMAR
FIFA Balllon d'Or ndio Tuzo ya ambayo hutunukiwa Mchezaji Bora Duniani kwa kila Mwaka kutokana na Kura za Makocha na Makepteni wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama wa FIFA pamoja na Jopo maalum la Wanahabari kutoka Jarida la France Football ambao ndio Waasisi wa Tuzo hii.
Kwa Miaka 7 iliyopita Mshindi wa Tuzo hii amekuwa ama Cristiano Ronaldo wa Real Madrid au Lionel Messi wa Barcelona.
Safari hii Wawili hao wapo tena kwenye 3 Bora ya Wagombea pamoja na Neymar wa Brazil.
Watatu hawa wote Makepreni wa Nchi zao, Ronaldo wa Oortugal, Messi wa Argentina na Neymar wa Brazil.

Watatu hawa ndio waliochujwa kutoka kwa Listi ya Washindani wa awali 23 na Leo, huko Zurich, Uswisi, mmoja wao ataibuka kidedea katika Hafla maalum.

YAFUATAYO NI MAFANIKO YAO KWA MWAKA 2015:
CRISTIANO RONALDO

- Anawania kuitwaa Tuzo hii kwa mara ya 3 mfululizo baada ya kuizoa 2013 na 2014.
-2015 hakutwaa Kombe lolote.
-Katika Raundi ya Pili ya Msimu wa 2014/15 alifunga Bao 29 na pia kuweka Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ta Real Madrid Mwezi Oktoba.
NEYMAR
-Hajawahi kutwaa Tuzo hii.
-Katika Raundi ya Pili ya Msimu wa 2014/15 alifunga Bao 24.
-Msimu huu anafungana kwa Ufungaji Bora wa La Liga akiwa na Bao 15.
LIONEL MESSI
-Ameshatwaa Tuzo hii mara 4.
-2015 yeye aliiongoza Barcelona kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
-Katika Raundi ya Pili ya Msimu wa 2014/15 alifunga Bao 28.