Saturday, January 2, 2016

FULL TIME: ARSENAL 1 v 0 NEWCASTLE UNITED, LAURENT KOSCIELNY AIPAISHA KILELENI ZAIDI GUNNERS LEO!

Laurent Koscielny ameifungia Arsenal Bao Dakika ya 72 na kuwapa ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Newcastle Uwanjani Emirates na kupaa Pointi 2 juu kileleni.
Newcastle walicheza vizuri na kustahili kuambua hata Sare lakini Arsenal wamepenya na kuwaacha Leicester City Pointi 2 nyuma baada ya Leicester kutoka 0-0 na Bournemouth.