Saturday, January 16, 2016

FULL TIME: CHELSEA 3 v 3 EVERTON

Mechi hii iliyochezwa Stamford Bridge ilikuwa 0-0 hadi Mapumziko na Kipindi cha Pili Everton walitangulia 2-0 kwa Bao za John Terry, aliejifunga mwenyewe, na Kevin Mirallas, Bao hizo zikifungwa Dakika za 50 na 56.
Lakini katika Dakika za 64 na 66, Chelsea walisawazisha kwa Bao za Diego Costa na Cesc Fabregas.
Hata hivyo, katika Dakika ya 90 na ushei, kizaazaa cha Kona kiliifanya Everton wapige Bao lao la 3 Mfungaji akiwa Ramiro Funes Mori alietokea Benchi.
Zikiwa zimeongezwa Dakika 7 za Majeruhi, Chelsea walisawazisha baada ya Dakika hizo 7 kumalizika kwa Bao ambalo lilionekana wazi ni Ofsaidi la Nahodha wao John Terry na kuwapa Sare ya 3-3.