Sunday, January 3, 2016

FULL TIME: CRYSTAL PALACE 0 v 3 CHELSEA, WILLIAN NA OSCAR WAIPA USHINDI BLUES LEO!

LEO Chelsea wamepata ushindi wao wa kwanza chini ya Meneja mpya Guus Hiddink ambae amerejea Klabuni hapo kwa mara ya pili baada ya kuichapa Crystal Palace Bao 3-0 Uwanjani Selhurst Park kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Bao za Chelsea zilifungwa na Emboaba Oscar, Dakika ya 29, baada ya pasi safi ya Diego Costa, Willian, Dakika ya 60 na Diego Costa Dakika 66.
Ushindi huu wa Leo umewapandisha Chelsea na kukamata Nafasi ya 14 kwenye Ligi.