Saturday, January 2, 2016

FULL TIME: MANCHESTER UNITED 2 v 1 SWANSEA CITY

Wayne Rooney Leo ameipa mguu mwema wa kuanza Mwaka Mpya wa 2016 alipoipa Manchester United ushindi kwa kufunga Bao la ushindi walipoifunga Swansea City 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England. Wayne Rooney akishangilia bao lake la ushindi la pili2-1Martial na Rooney wakipongezanaRooney
Ushindi huu, ambao ni wa kwanza katika Mechi 8, umeipandisha Man United hadi Nafasi ya 5.
Bao za Man United zilifungwa na Anthony Martial Dakika ya 47 na Swansea
kurudisha Dakika ya 70 kwa Bao la Gylfi Sigurdsson lakini Wayne Rooney, akipokea pasi safi ya Martial, alifunga Bao la ushindi kwa kisigino katika Dakika ya 77.
Bao hilo limemfikisha Rooney Nafasi ya Pili katika Ufungaji Bora kwenye Ligi Kuu England, akiwa nyuma ya Alan Shearer na pia Nafasi ya Pili katika Ufungaji Bora katika Historia ya Man United akiwa na Bao 238, Bao 11 nyuma ya Mshikilia Rekodi, Sir Bobby Charlton.