Saturday, January 2, 2016

FULL TIME: WEST HAM UNITED 2 v 0 LIVERPOOL, KILIO LEO KWA MAJOGOO!! KLOPP ALILIA KIPIGO KILICHOWASHUSHA NAFASI YA 9

BAO 2 za Michail Antonio na Andy Carroll zimewapa ushindi West Ham walipocheza na Liverpool Uwanjani Upton Park katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England kwa Mwaka 2016.
Ushindi huu umewarusha West Ham kuwa juu ya Liverpool kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Nafasi ya 5 na Liverpool kuporomoka hadi Nafasi ya 9 na Misimamo hii huenda ikabadilika baadae Leo kutokana na matokeo ya Mechi nyingine.

Hadi Mapumziko, West Ham walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 10 la Antonio na Carroll, Mchezaji wa zamani wa Liverpool, kupiga la pili Dakika ya 55.