Sunday, January 17, 2016

FULL TIME: YANGA 1 v 0 NDANDA FC


MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, wametwaa uongozi wa Ligi baada ya kuichapa Ndanda FC 1-0 katika Mechi pekee ya Ligi iliyochezwa Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Yanga sasa wana Pointi 36 kwa Mechi 14 sawa na Azam FC lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli kwani wamefunga Bao 31 na kufungwa 5, hivyo tofauti yao ya Magoli ni 26 wakati Azam FC wamefunga 28 na kufungwa 9 wakiwa na tofauti ya Magoli 19.
Bao pekee la Yanga hii Leo lilitokana kwa Penati iliyopigwa na Kevin Yondani katika Dakika ya 60 na ilitolewa kufuatia Deus Kaseke kuchezewa Faulo na Hemed Koja.