Monday, January 25, 2016

HALI NI TETE KWA MENEJA LOUIS VAN GAAL NDANI YA KLABU YA MAN UNITED, MASHABIKI WAMKALIA KOONI!! WOODWARD ATETA NA WACHEZAJI WAANDAMIZI KWENYE KIKAO. JOSE MOURINHO AVIZIA KAZI OLD TRAFFORD!

Siku zinahesabika za Van GaalManchester United manager Louis Van Gaal looks dejectedKuna Habari zimevuja huko England kuwa sasa Louis van Gaal yupo ukingoni kuondoka Manchester United huku Mazoezi yaliyopangwa Jumapili na Jumatatu kufutwa na Mtendaji Mkuu, Ed Woodward, akifanya Kikao cha dharura na Wachezaji Waandamizi pamoja na Viongozi wengine wa juu Klabuni hapo.
Habari za ndani zimedai Van Gaal alikutana na Woodward Jumapili na kisha kuruka kwenda kwao Netherlands kuhudhuria kile kilichoitwa Bethdei ya Binti wake wa Kike.
Lakini hali Klabuni hapo ni tete hasa kutokana na presha ya Mashabiki wa Klabu hiyo ambao Jumamosi walimzomea Van Gaal na kumtaka aondoke mara baada ya kufungwa 1-0 na Southampton Uwanjani Old Trafford.
Hicho kilikuwa kipigo chao cha 6 kwenye Ligi Kuu England Msimu huu na kimewatupa Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City na Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 ambayo ndiyo nafasi ya mwisho ya kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Mbali ya kufungwa, Mashabiki wa Man United hawaridhishwi na staili ya uchezaji ya Van Gaal ambae msisitizo wake ni Difensi.
Huku Van Gaal akitarajiwa mwenyewe kubwaga manyaga badala ya kufukuzwa, zipo kila dalili Jose Mourinho huenda akachukua hatamu hasa baada ya kuvuja habari kuwa Mreno huyo aliandika Barua ya Kurasa 6 kwa Man United akielezea kufaa kwake kuongoza Timu hiyo.

Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes, amekanusha kuwepo kwa Barua hiyo na kudai ni upuuzi lakini Waendesha Kamari huko Uingereza wemweka Mourinho kuwa ndie Meneja mpya wa Manchester United.