Saturday, January 9, 2016

LA LIGA: REAL MADRID UWANJANI LEO....MENEJA WAKE MPYA ZIDANE KUANZA RASMI KIBARUA BENARBEU DHIDI YA DEPORTIVO

KOCHA MKUU MPYA wa Real Madrid, Lejendari wa France, Zinedine Zidane, Leo kwa mara ya kwanza kabisa ataiongoza Timu yake itakapocheza Mechi ya La Liga Uwanjani Santiago Bernabeu dhidi ya Deportivo La Coruna.
Zidane aliteuliwa kuwa Kocha wa Real mapema Wiki hii kumrithi Rafael Benitez aliefukuzwa baada ya Miezi 7 tu katika wadhifa wake.
Kabla ya uteuzi wake, Zidane, ambae aliwahi kuwa Mchezaji wa Real katika ya 2006 na 2011, alikuwa Msaidizi wa Kocha Carlo Ancelotti wakati alipokuwa akiifundisha Real na kisha Mwezi Juni Mwaka Jana Zidane akafanywa Kocha wa Timu ya Real B iitwayo Castilla.
Hivi sasa Real wapo Nafasi ya 3 kwenye La Liga wakiwa Pointi 2 nyuma ya Barcelona na Pointi 4 nyuma ya Vinara Atletico Madrid.
LA LIGA
RATIBA
Jumamosi Januari 9

18:00 FC Barcelona v Granada CF
20:15 Sevilla FC v Athletic de Bilbao
20:15 Getafe CF v Real Betis
22:30 Real Madrid CF v Deportivo La Coruna

Jumapili Januari 10
00:05 Levante v Rayo Vallecano
14:00 Villarreal CF v Sporting Gijon
18:00 Real Sociedad v Valencia C.F
20:15 SD Eibar v RCD Espanyol
20:15 Las Palmas v Malaga CF
22:30 Celta de Vigo v Atletico de Madrid