Monday, January 18, 2016

LA LIGA: SUAREZ APIGA HAT-TRICK BARCA IKIINYUKA ATHLETIC DE BILBAO BAO 6-0!

NDANI ya NOU CAMP  ilishuhudiwa mvua ya Magoli wakati Barcelona inaitandika timu iliyokuwa punguu Mtu 10 Athletic Bilbao Bao 6-0 katika Mechi ya La Liga.
Balaa kwa Bilbao ilianza Dakika ya 4 tu baada ya Kipa wao Gorka Iraizoz Moreno kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumwangusha Luis Suarez na pia kutolewa Penati iliyofungwa na Lionel Messi.

Neymar akafunga Bao la Pili na Barca kwenda Haftaimu wakiwa 2-0 mbele.
Kipindi cha Pili, Luis Suarez alipiga Hetitriki na Ivan Rakitic akaongeza 1 na Barca kushinda 6-0.
Nao Atletico Madrid, wakicheza Ugenini, waliichapa Las Palmas 3-0 na kuzidi kuendelea kuongoza La Liga wakiwa na Pointi 47 kwa Mechi 20 wakifuata Barca wenye Pointi 45 kwa Mechi 19 na kisha Real wenye Pointi 43 kwa Mechi 20.
Messi alionesha Tuzo yake ya FIFA Ballon d"OrMessi kipenzi cha MashabikiBalaa lilianzia hapa kwa Kipa na SuarezKipa alimwaga Suarez Chini mapema dakika ya 4 baada ya beki nae kumkosaKipa wa Athletico de Bilbao alioneshwa kadi nyekunduMessi alianza kuonesha mambo yake kwenye mkwaju wa penatiMessi akiachia shuti kali kumfunga kipa wa De Bilbao