Sunday, January 3, 2016

LA LIGA: VALENCIA 2 - 2 REAL MADRID, PACO ALCACER AIBANA REAL NA KUGAWANA POINTI!

Paco Alcacer celebrates after  he scores a late equaliser for Valencia to earn a pointPaco Alcacer akishangilia baada ya kuisawazishia bao dakika za majeruhi na kufanya 2-2Real Madrid bao limefungwa na Karim Benzema dakika ya 16'
Valencia CF 1, Real Madrid 1. Daniel Parejo wa (Valencia CF) aliifanikishia bao kwa mkwaju wa penati na kwenda mapumziko kwa bao 1-1.


Alcacer akipongezwa na mwenzie Andre Gomes

Bao hilo liliwafanya wagawane pointi na Real Madrid

Wachezaji wa Valencia wakishangilia na kupongezana

Gareth Bale alifunga bao la kichwa na kufanya 2-1 dhidi ya Valencia

Patashika Bale akitupia

Valencia, Kikosi cha Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Garry Neville, Jana kilimudu kutoka Sare ya 2-2 na Miamba ya Spain Real Madrid katika Mechi ya La Liga iliyochezwa Estadio Mestalla huku Atletico Madrid wakitwaa uongozi wa Ligi hiyo baada ya kuifunga Levante 1-0 Juzi Jumamosi.
Real walitangulia kufunga katika Dakika ya 10 kwa Bao la Karim Benzema na Valencia kusawazisha Dakika ya 45 kwa Penati ya Daniel Parejo.

Bale alizungukwa kupongezwa na Wana Real.
Katika Dakika ya 68 Real walibaki Mtu 10 pale Mateo Kovacic alipoewa Kadi Nyekundu lakini hilo halikuwazuia Real kufunga Bao la Pili katika ya 82 kupitia Gareth Bale, Bao lilidumu Dakika 1 tu kwani Paco Alcacer alifunga Bao la kusawazisha na kuwapa Valencia Sare ya 2-2.
Matokeo hayo yamewaacha Real wakiwa Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Barcelona, ambao wamecheza Mechi 1 pungufu, huku Atletico Madrid wakiongoza wakiwa na Pointi 41 zikiwa ni Pointi 2 mbele ya Barcelona.