Tuesday, January 19, 2016

LEO HII...EMIRATES FA CUP: MARUDIO RAUNDI YA 3, JUMATANO LIVERPOOL V EXETER, LEICESTER V SPURS

WAKATI DROO na Ratiba ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP imeshafanyika, Leo Usiku na Jumatano zipo Mechi za Marudiano za Raundi ya 3 kwa Timu zilizotoka Sare.
Miongoni mwa hizo za Marudio ni ili ambayo itachezwa Villa Park ambako Aston Villa watarudiana na Timu ya Ligi 2, Wycombe, ambayo walitoka Sare 1-1 hapo Januari 9.
Jumatano, huko Anfield, Liverpool wanarudiana na Timu ya Ligi 2, Exeter, baada ya kutoka nayo 2-2 huko Exter City hapo Hanuari 8.
Siku hiyo hiyo, huko King Power Stadium, Leicester City, Timu ambayo ipo kileleni mwa Ligi Kuu England, itarudiana na Tottenham baada ya kutoka 2-2 huko White Hart Lane.
Hii itakuwa mara ya 3 kwa Timu hizi kukutana baada ya Juzi pia Leicester kuichapa Tottenham 1-0 huko White Hart Lane kwenye Ligi.
Dondoo muhimu:
-FA CUP sasa inaitwa EMIRATES FA CUP kutokana na Udhamini wa Shirika la Ndege la Falme za Nchi za Kiarabu, Emirates.
-Emirates sasa wanadhamini FA CUP kwa Miaka Mitatu.


EMIRATES FA CUP
Marudiano-Raundi ya 3
Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumanne Januari 19

Aston Villa v Wycombe
Bolton v Eastleigh
Bradford v Bury
Bristol City v West Brom
MK Dons v Northampton
Portsmouth v Ipswich
Yeovil v Carlisle
23:00 Reading v Huddersfield

Jumatano Januari 20
Leicester v Tottenham
23:00 Liverpool v Exeter (2000 GMT)