Sunday, January 31, 2016

FULL TIME: EMIRATES FA CUP: MK DONS 1 v 5 CHELSEA, OSCAR APIGA HAT-TRICK KIPINDI CHA KWANZA!


Hat-tric ya Oscar, Bao la Eden Hazard la Penati, ikiwa ni Bao lake la kwanza katika Mechi 28, na lile la Bertrand Traore, limewapa Chelsea ushindi wa 5-1 walipocheza na MK Dons katika Mechi ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP iliyochezwa huko mk Denbigh Stadium, Mjini Milton Keynes.
Mapema Leo, Everton nao walitinga Raundi ya 5 kwa kushinda Ugenini kwa kuichapa Carlisle 3-0 kwa Bao za Arouna Kone, Aaaron Lennon na Ross Barkley.
Sasa Chelsea na Everton zinaungana na Timu nyingine 16 [zikiwemo zile za Mechi kurudiwa baada ya Sare] kwenye Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 5 itakayofanyika baadae leo.

Bao la 4 limefungwa Eden Hazard dakika ya 55 kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati huku Bertrand Traore akifunga bao la 5 dakika ya 62'
Milton Keynes Dons bao lake la pekee limefungwa na
Darren Potter dakika ya 21' 

Chelsea walipatiwa bao tatu zote zikifungwa na Oscar kipindi cha kwanza.
• Oscar 15'
• Oscar 32'
• Oscar 44