Wednesday, January 13, 2016

SPANISH COPA DEL REY: ESPANYOL 0 v 1 BARCELONA, (1 - 6 Agg), MUNIR EL HADDADI AIPA USHINDI BARCA SASA WAKO ROBO FAINALI!

Munir El Haddadi  alifunga dakika ya 32 Na bao la pili lilifungwa pia na Munir El Haddadi dakika ya 88 na kufanya mtanange kumalizika 2-0. Ikiwa ni jumla ya mabao
(Agg 1-6).
Chipukizi  wa Barcelona Munir El Haddad  alipiga Bao 2 na kuipa Timu yake ushindi wa 2-0 dhidi ya Espanyol na kuwawezesha kutinga Robo Fainali ya Copa del Rey.
Barca wamesonga kwa jumla ya Mabao 6-1 baada ya kuwatwanga Espanyol, ambao ni Mahasimu wao wa Jiji la Barcelona 4-1 katika Mechi ya kwanza.
Lionel Messi, ambae alicheza Dakika zote 90 kwenye Mechi hii ambayo Barca walipumzisha Mastaa kadhaa, alimtengenezea El Haddad Bao la kwanza ambalo alilifunga Dakika ya 32.
El Haddad, ambae alichezeshwa kumbadili Luis Suarez aliefungiwa Mechi 2, alifunga Bao la Pili Dakika ya 88.
Barca ndio Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey.