Sunday, January 24, 2016

FULL TIME: ARSENAL 0 v 1 CHELSEA, DIEGO COSTA AONGEZA MASAA YA UKAME WA BAO KWA GUNNERS KWA KUIPA BLUES USHINDI!

Arsene Wenger na Wasaidizi wake wakiwa hoi kwenye benchi!Wachezaji wa Chelsea wakimzunguka Diego kumpongeza kwa baoJohn Terry nae akifurahia huku akionekana kwamba Timu yao ikikazana yaweza kupanda nafasi ya nne
Diego akishangilia bao lake dakika ya 23
Diego Costa, ameacha gumzo kubwa baada ya kusababisha Sentahafu wa Arsenal apewe Kadi Nyekundu katika Dakika ya 18 na yeye kuifungia Chelsea Bao pekee na la ushindi katika Dakika ya 23.Kipigo hiki cha 1-0 cha Chelsea kwa Arsenal ni muendelezo wa vipigo mfululizo kuanzia 2010 lakini Leo ndio cha kuuma sana kwani kimewatupa Arsenal Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa nyuma ya Vinara Leicester City na Man City.
Arsenal, wakiwa kwao Emirates, walipata balaa Dakika ya 18 tu baada ya Sentahafu wao, Per Mertesacker, kumwangusha Diego Costa aliekuwa akichanja mbuga kumuona Kipa na Refa Mark Clattenburg kuamua ni Kadi Nyekundu ingawa tukio hili limegawa pande kila Mtu akibaki na nini alichoona yeye.

Upungufu huo ulimfanya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amtoe Straika Olivier Giroud, na kumwingiza Sentahafu Mbrazil Gabriel Paulista ambae ndie alitoa uchochoro Dakika 5 baadae kwa Diego Costa kufunga Bao pekee na la ushindi.
Chupuchupu!!
Chelsea wanaongoza bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Arsenal bao likifungwa na Diego Costa dakika ya 23 kipindi cha kwanza.
Per Mertesacker ameoneshwa kadi nyekundu na sasa Arsenal wanacheza pungufu 10 Uwanjani