Sunday, January 3, 2016

FULL TIME: EVERTON 1 v 1 TOTTENHAM HOTSPURS, HAKUNA MBABE LEO NDANI YA GOODSON PARK!

1-1 Mtanange umemalizika dakika 90 huku Spurs wakiumaliza kwa staili ya aina yake!
Everton na Tottenham Leo zimetoka Sare ya 1-1 Uwanjani Goodison Park katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Matokeo haya yamewabakisha Tottenham Nafasi 4 na Everton wapo Nafasi ya 11.

Everton ndio waliotangulia kufunga kwa Shuti kali la Mchezaji wa zamani wa Tottenham, Aaron Lennon, katika Dakika ya 22 lakini Tottenham wakasawazisha katika Dakika ya 46 kupitia Dele Alli alieweka gambani Krosi ndefu ya Toby Alderweireld na kufumua Shuti lililomshinda Kipa Tim Howard.Lennon 1-0Lukaku kaanza kwa Everton