Sunday, January 10, 2016

FA CUP: CHELSEA 2 v 0 SCUNTHORPE


Chelsea imetinga Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP baada ya kuifunga Timu ya Daraja la chini la Ligi 1 Scunthorpe United Bao 2-0 kwenye Mechi iliyochezwa Stamford Bridge.
Bao za Chelsea zilifungwa na Diego Costa na Ruben Loftus-Cheek alieingizwa kutoka Benchi.
Katika Mechi ya kwanza hii Leo, Oxford United, Klabu inayocheza Ligi 2, ilitoka nyuma kwa Bao 1 na kuitwanga Swansea City, inayocheza Ligi Kuu England, Bao 3-2.
Bao za Oxford zilifungwa na Liam Sercombe, Penati Dakika ya 45, na nyingine 2 na Kemar Roofe katika Dakika za 49 na 59.
Bao za Swansea zilipachikwa na Jefferson Montero na Bafetimbi Gomes katika Dakika za 23 na 66.
Droo ya Mechi za Raundi ya 4 itafanyika Jumatatu Usiku.

Scunthorpe