Sunday, January 10, 2016

FULL TIME: MAPINDUZI CUP: SIMBA 0 v 1 MTIBWA SUGAR, MNYAMA SIMBA ATUNGULIWA ZENJ! ATUPWA NJE!


Simba wamelelala 1-0 mbele ya Timu ya Mtibwa kwenye mchezo wa Nusu Fainali
za Mapinduzi Cup kwenye Uwanja wa Amaan Stadium Zanzibar. Bao limefungwa dakika ya 45 kipindi cha kwanza. BAO la Ibrahim Rajab limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar walipoichapa Simba katika Mechi ya Nusu Fainali Mapinduzi Cup iliyofanyika huko Amaan Stadium Zanzibar.
Kipigo hiki kimewavua Simba Ubingwa wa Kombe hili ambalo walilitwaa Mwaka Jana walipoitoa Mtibwa Sugar kwa Penati 4-3 kwenye Fainali.
Mtibwa Sugar sasa wametinga Fainali na watacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine itakayochezwa Usiku huu kati ya Yanga na URA ya Uganda.NUSU FAINALI za Mapinduzi Cup zinachezwa huko Amaan Stadium Zanzibar kwa Mabingwa Watetezi Simba kuanza kucheza na Mtibwa Sugar na baadae Yanga kuivaa URA ya Uganda.
Yanga na Simba zote zilitwaa ushindi wa Makundi yao kw azote kushinda Mechi 2 na Sare moja wakati Mtibwa Sugar na URA zikishika Nafasi za Pili.
Fainali ya Mashindano haya itafanyika Jumatano hapo hapo Amaan Stadium.
Mechi ya Leo ya Simba na Mtibwa Sugar inazikutanisha Timu ambazo zilikutana Fainali Mwaka Jana na Simba kuibuka kidedea kwa Penati 4-3.