Sunday, January 17, 2016

FULL TIME: LIVEPOOL 0 v 1 MANCHESTER UNITED, KEPTENI WAYNE ROONEY AIPA USHINDI UNITED LEO ANFIELD NA KUWEKA REKODI MPYA!

BAO la Kepteni Wayne Rooney, la kwanza kabisa Uwanjani Anfield tangu 2005, Leo limewapa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mahasimu wao Liverpool katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Liverpool walitengeneza nafasi nyingi katika Mechi hii lakini Kipa David De Gea na umaliziaji wao mbovu ndio vilikuwa vikwazo na Man United kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 78 kwa Shuti lao pekee katika Mechi nzima lililolenga Golini.
Goli hilo lilitokana na Kona ambapo Marouane Fellaini alipiga Kichwa kilichogonga Posti na Mpira kuwahiwa na Wayne Rooney na kutinga.
Hilo ni Bao lake la 5 katika Mechi 4 zilizopita na ni la 176 kwenye Ligi Kuu England ambalo limemfanya sasa awe anashikilia Rekodi ya kuwa Mfungaji wa Bao nyingi kwenye Ligi Kuu England akichezea Klabu 1 tu akifuatiwa na Thierry Henry mwenye 175 alizofunga akiiichezea Arsenal pekee.
Matokeo haya yameipandisha Man United Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Timu ya 4 Tottenham wakati Liverpool wapo Nafasi ya 9 Pointi 8 nyuma ya Tottenham.
Rooney dakika ya 78 kafunga bao na kuitangulizia bao la kuongoza Man United kwa kufanya 1-0 dhidi ya Wenyeji Liverpool. Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya mwisho na Man United kuibuka kidedea. Bao hilo pia limemfanya aweke rekodi mpya kwa Klabu yake ya Man United kwa kufikisha bao 176 akifuatiwa na aliyekuwa na rekodi ya mabao 175.De Gea akishangilia bao hilo la Rooney1-0Hatari tupu Rooney akishangilia bao lake la 176 kwa Man UnitedJuan Mata na kipa David De GeaMartial akiwachambua Liverpool