Friday, January 8, 2016

LUIS SUAREZ AFUNGIWA MECHI MBILI

Luis Suarez amefungiwa Mechi 2 kufuatia rabsha zilizotokea baada ya Mechi ya Barcelona na Mahasimu wao wa Mjini Barcelona, Espanyol, Uwanjani Nou Camp baada ya Mechi yao ya Copa del Rey kumalizika.
Suarez, Straika wa Uruguay mwenye Miaka 28, anadaiwa kuwavaa na kuwatisha Wachezaji wa Espanyol kufuatia Mechi ambayo Barca walishinda 4-1 Juzi Jumatano.
Kifungo cha Suarez ni kwa Mechi za Copa del Rey tu na hivyo ataikosa Mechi ya Marudiano na Espanyol Jumatano ijayo lakini Klabu yake imeamua kukata Rufaa kupinga Kifungo hiki.
Barca imedai kuwa Suarez hakutumia lugha chafu katika mzozo huo wa baada ya Mechi kama Ripoti ya Refa inavyodai.
Kwenye Mechi hiyo, Espanyol walimaliza wakiwa Mtu 9 baada ya Wachezaji wao, Hernan Perez na Pape Diop, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.