Thursday, January 21, 2016

REAL JUU, BARCELONA 2, MAN UNITED WA 3

KWA mujibu wa Listi iliyochapishwa Leo na Deloitte, Magwiji wa Mahesabu, Klabu za Spain, Real Madrid na Barcelona, zikifuatiwa na Manchester United, ndizo zinazoongoza Duniani kwa Mapato kwa Mwaka 2014/15.
Lakini, kwa mujibu wa Deloitte, Man United inatarajiwa kutwaa uongozi wa Listi hiyo baadae Mwakani licha ya kutofika hatua za Mtoano za UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu huu.
Hali hiyo itakuja kutokana na Man United kuanza kukomba Mapato yatokanayo na Ufadhili wa Adidas wa Miaka 10 wa Jezi zao na pia ile Dili na Chevrolet.
Kwa Mwaka 2014/15, Man United wameshuka kutoka Nafasi ya Pili hadi ya 3 na ni miongoni mwa Klabu 9 za Ligi Kuu England ambazo zipo kwenye 20 Bora.
West Ham imetinga kwenye Listi hiyo ya 20 Bora kwa mara ya kwanza kabisa.

 
Mapato ya Man United yalishuka kutoka from £433.2m kwa Mwaka 2013-14 kwenda £395.2m kutokana na kutocheza UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kipindi hicxho.
Lakini, Meneja mwandamizi wa Deloitte, Tim Bridge, anaamini Man United iko imara kibiashara.
Nyuma ya Man United, kwenye Nafasi ya 6, wapo Man City wakifuatiwa na Arsenal, Chelsea na Liverpool,
Klabuni nyingine za England ambazo zimo 20 Bora ni Tottenham, Everton
Newcastle na West Ham.