Saturday, January 16, 2016

MANCHESTER CITY 4 vs 0 CRYSTAL PALACE, DELPH, SERGIO AGUERO NA SILVA WAIPA USHINDI CITY NA KUINYANYUA HADI KILELENI LEO!

Wakiwa kwao Etihad, Man City Leo wameirarua Crystal Palace Bao 4-0 na kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England pengine kwa muda tu hadi Leicester City watakapocheza baadae Usiku huu.
Sare au ushindi kwa Leicester, wanaocheza Ugenini na Aston Villa, utawaweka kileleni.

Bao za City hii Leo zilifungwa na Fabian Delph, Sergio Aguero, Bao 2, na David Silva.