Sunday, January 3, 2016

MAPINDUZI CUP 2016: YANGA YAANZA KWA KISHINDO! YAICHAPA MAFUNZO BAO 3-0.

MAPINDUZI CUP 2016 imeanza rasmi Leo kwa Mechi ya Kundi B kati ya Yanga na Mafunzo ya Zanzibar na Yanga kuibuka na ushindi wa Bao 3-0 kwenye Mechi iliyochezwa huko Zanzibar Uwanja wa Amaan.
Katika Mechi hiyo, Yanga ilifunga Bao zake kupitia Donald Ngoma, aliefunga Bao 2, na Paul Nonga kufunga moja.
Baadae Leo, Mechi nyingine ya Kundi B itachezwa kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC hapo hapo Uwanjani Amaan.

MAKUNDI:
KUNDI A:
Simba, Jamhuri, JKU, URA
KUNDI B: Yanga, Mafunzo, Azam FC, Mtibwa Sugar

Kundi A, ambalo lina Timu za Simba, ambao ni Mabingwa Watetezi, Jamhuri na JKU za Zanzibar, na Timu ngeni pekee, URA ya Uganda, zitaanza Mechi zake Jumatatu Januari 4 kwa JKU kucheza na URA Jioni na Usiku ni Simba na Jamhuri.
Washindi Wawili wa juu wa kila Kundi watasonga Nusu Fainali.

RATIBA/MATOKEO:
Mechi zote kuchezwa Amaan Stadium, Zanzibar
Jumapili Januari 3

Yanga 3 v  Mafunzo 0
20:15 Mtibwa Sugar v Azam FC

Jumatatu Januari 4
16:15 JKU v URA
20:15 Simba v Jamhuri

Jumanne Januari 5
1615 Mafunzo v Mtibwa Sugar
2015 Azam FC v Yanga

Jumatano Januari 6
1615 Jamhuri v JKU
2015 URA v Simba

Alhamisi Januari 7
1615 Azam FC v Mafunzo
2015 Mtibwa Sugar v Yanga

Ijumaa Januari 8
1615 Jamhuri v URA
2015 Simba v JKU

Nusu Fainali
Jumapili Januari 10

1615 Mshindi A v Wa Pili B
2015 Mshindi B v Wa Pili A

Fainali
Jumatano Januari 13