Wednesday, January 13, 2016

URA MABINGWA WAPYA MAPINDUZI CUP 2016: MTIBWA SUGAR 1 v 3 URA, JULIUS NTAMBI NA PETER LWASSA WAIPA USHINDI!

Bao Julius Ntambi dakika ya 16 kipindi cha kwanza aliipachikia bao la kuongoza kwa kufanya 1-0 dhidi ya Timu ya Mtibwa Sugar. 

Bao hilo lilipatikana kwa kupigwa mpira kama kona na mchezaji wa Timu ya URA kuugonga kwa kichwa kuelekea langoni na Ntambi kuumalizia kwa kichwa nyavuni na kuwaacha mabeki wa Timu ya Mtibwa kubaki wakiduwaa na kushanga.

Sasa ni kipindi cha pili kinaendelea...Sasa ni 2-0 kupitia kwa Peter Lwassa na baadae aliifungia bao la tatu na kufanya 3-0 Akifunga dakika ya 85 na dakika ya 88. 

Mtibwa Sugar walipata bao lao dakika ya 90 kupitia kwa Jaffar Salum baada ya kipa wao kufanya makosa ya kizembe na mtanange kumalizika kwa bao 3-1.URA ya Uganda wamebeba Mapinduzi Cup baada ya kuitwanga Mtibwa Sugar ya Tanzania Bao 3-1 katika Fainali iliyochezwa Jana Usiku huko Amaan Stadium, Zanzibar.


Mbali ya kutwaa Kombe, URA pia wamepewa Shilingi Milioni 10 kama Mabingwa na Mtibwa Sugar kupata Shilingi Milioni 5 kama Washindi wa Pili.