Sunday, January 10, 2016

PAUL SCHOLES AMPASHA VAN GAAL - ‘TIMU HAINA MVUTO, HAIVUTII!’ ....INA BOA!

KWA mara nyingine tena, Lejendari wa Manchester United Paul Scholes amemshambulia Louis van Gaal na Timu yake Manchester United kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Timu ya Daraja la chini Ligi 1 Sheffield United kwenye Raundi ya 3 ya FA CUP katika Mechi iliyochezwa Old Trafford Jumamosi.
Scholes amekuwa akiponda staili ya uchezaji ya Man United na Jana pia alijitokeza na kumponda Mdachi huyo baada ya kuhitaji Penati ya Dakika za Majeruhi ya Wayne Rooney ili kuifunga Sheffield United ambayo iko Daraja la chini.

Kabla ya Bao hilo la Dakika ya 93, Mamia wa Mashabiki wa Man United walionekana wakitoka nje ya Old Trafford kwa hasira.
Scholes ameeleza: “Wachezaji walionekana wamepooza, doro. Hamna ari, hakuna Mchezaji anaemsakama mwenzake, hawacheki, hamna mvuto. Nadhani hata Van Gaal mwenyewe kwenye Benchi anaonekana kupooza lakini atajitokeza na kusema amefurahi!”
Aliongeza: “Hawakucheza vizuri. Je Van Gaal atafurahishwa na hilo? Pengine. Nadhani hivyo ndivyo anavyotaka Timu yake icheze.
Hatujaona jipya katika Miezi 6, hivi ndivyo Timu zake hucheza Soka na atafurahishwa na ushindi wa 1-0. Hawakutengeneza nafasi na imebidi washinde Gemu na Timu ya Ligi 1 kwa Penati ya Dakika ya 94. Kwa hakika, hali si njema!”