Wednesday, January 13, 2016

PAUL SCHOLES BADO AENDELEA KUICHAMBUA MAN UNITED! ASEMA BORA AU AFADHALI KULIKO WALIVYOCHEZA NA SHEFFIELD!

Paul Scholes ameelezea uchezaji wa Manchester United walipotoka Sare 3-3 na Newcastle Jana huko Saint James Park katika Mechi ya Ligi Kuu England kuwa ni afadhali kuliko Mechi zao za hivi karibuni.
Kwenye Mechi ya kabla na Newcastle, walihitaji Penati ya Dakika ya 94 ili kuitoa Timu ya Daraja la chini Sheffield United ili kushinda 1-0 kwenye Mechi hiyo ya FA CUP na Scholes aliponda sana staili ya Meneja Louis van Gaal.

Jana, mara baada ya Sare ya 3-3 ambayo Newcastle walirudisha Bao katika Dakikabya 90, Scholes, akiongea kwenye TV ya BT SPORT, alisema: "Hiyo ilikuwa afadhali kwa mbali. Kawaida kwenda kuitazama Manchester United ni burudani hata kama wanafungwa Mabao na wao kupachika Mabao."
"Usiku huu ilikuwa kama tunaiona Manchester United halisi. Wangeweza kushinda kama Kichwa cha Fellaini kingefanya 4-2 au Lingard angetumia vyema nafasi alopata!"
Mechi inayofuata ya Ligi kwa Man United ni Jumapili ijayo huko Anfield.