Saturday, January 30, 2016

RATIBA - LA LIGA KWA WIKIENDI HII: JUMAMOSI NI NOU CAMP BARCELONA vs ATLETICO MADRID. JUMAPILI NI REAL MADRID v ESPANYOL

WIKIENDI hii huko Spain kwenye La Liga, Mechi yenye mvuto mkubwa ni ile itakayochezwa huko Nou Camp kati ya Mabingwa wa Spain Barcelona na Atletico Madrid.
Timu hizi zinafungana kileleni mwa La Liga zikiwa na Pointi sawa lakini Barca wako juu ya Atleti kwa ubora wa Goli na pia rekodi yao ya kuifunga Atleti 2-1 Mwezi Septemba katika Mechi yao ya kwanza ya La Liga Msimu huu.

Hali za Timu
Barcelona watakuwa nae tena Gerard Pique ambae alikuwa kifungoni lakini Jordi Alba bado ni majeruhi na huenda asicheze.
Atleti watawakosa majeruhi Tiago na Fernando Torres wakati Angel Correa akiwa kifungoni.
LA LIGA- RATIBA
Januari 30

18:00 FC Barcelona v Atletico de Madrid
20:15 Getafe CF v Athletic de Bilbao
20:15 SD Eibar v Malaga CF
22:30 Villarreal CF v Granada CF

Jumapili Januari 31
00:05 Real Sociedad v Real Betis
14:00 Sevilla FC v Levante
18:00 Valencia C.F v Sporting Gijon
20:15 Las Palmas v Celta de Vigo
22:30 Real Madrid CF v RCD Espanyol

Jumatatu Februari 1
22:30 Deportivo La Coruna v Rayo Vallecano