Tuesday, January 12, 2016

RATIBA: LIGI KUU ENGLAND KUENDELEA TENA LEO JUMANNE NA JUMATANO.

LIGI KUU ENGLAND ipo tena dimbani kati-wiki na Jumanne Usiku zipo Mechi 3 na Jumatano Usiku kuchezwa 7.
Mechi za Jumanne Usiku ni kule Villa Park kati ya Aston Villa na Crystal Palace, Bournemouth kuwa Nyumbani kuivaa West Ham na mvuto mkubwa ni huko Saint James Park wakati Newcastle, ambao sasa wako hali mbaya, wakicheza na Man United isiyotabirika na ambayo imekuwa kero kubwa kwa Mashabiki wake ambao wengi wao washamchoka Meneja wao Mdachi, Louis van Gaal.
Licha ya kuanza Mwaka mpya kwa kushinda Mechi zao zote 2 lakini jinsi Timu inavyocheza imewahuzunisha wengi hasa kwa vile Mechi hizo 2 walizoshinda ni ushindi finyu na wa kwanza katika Mechi zao 10 zilizopita.
Mwendo huo umewafanya Mwezi Desemba wapoteze Pointi 13 za Ligi Kuu England na kuwaporomosha hadi Nafasi ya 5.
Hata hivyo, Man United wana rekodi nzuri huko Saint James Park baada ya kushinda Mechi zao 3 zilizopita na sasa wanapambana na Newcastle, ambayo ipo chini ya Steve McClaren, Meneja Msaidizi wa zamani chini ya Sir Alex Ferguson, ambayo taabani ikiwa imefungwa Mechi zao 4 zilizopita kwa Bao 1-0 kila moja na kuachwa Nafasi ya 3 toka mkiani.

RATIBA:
Jumanne Januari 12
[Mechi zote Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Aston Villa v Crystal Palace
Bournemouth v West Ham
Newcastle v Man United

Jumatano Januari 13
[Mechi zote Saa 4 Dakika 45 Usiku]

Chelsea v West Brom
Man City v Everton
Southampton v Watford
Stoke v Norwich
Swansea v Sunderland

[Mechi zote Saa 5 Usiku]
Liverpool v Arsenal
Tottenham v Leicester