Saturday, January 9, 2016

TFF YAWASHUKURU WATANZANIA KWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUMPOKEA MBWANA SAMATTA SAA NANE USIKU

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru watanzania wote, wapenzi, na wadau wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza usiku saa 8 uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es salam kumpokea mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani Mbwana Samatta. Samatta alipokelewa na viongozi wa serikali, TFF, familia yake wakiwemo baba na mama yake mzazi na watanzania wengi walijitokeza kumlaki mchezaji huyo. Mara baada ya mapokezi ya uwanja wa ndege, TFF ilimpeleka moja kwa moja kupumzika katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam.