Wednesday, January 13, 2016

UHAMISHO JANUARI 2016: NEWCASTLE YAMNUNUA JONJO SHELVEY KWA PAUNI MILIONI 12

Kiungo wa Swansea City, Jonjo Shelvey, Leo anapimwa afya huko Newcastle ili kukamilisha Uhamisho wake wa Pauni Milioni 12.
Huyu anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Meneja Steve McClaren katika kipindi hiki baada ya pia kumsaini Henri Saivet kutoka Bordeaux kwa Mkataba wa Miaka Mitano na Nusu kwa Dau ambalo halikutajwa.
Shelvey, mwenye Miaka 23, alisainiwa na Swansea Julai 2013 kutoka Liverpool kwa Pauni Milioni 5 na kuichezea Swansea Mechi 77 na kufunga Bao 9.