Wednesday, January 13, 2016

UHAMISHO JANUARI: LIVERPOOL YAMSAINI STEBEN CAULKER MKOPO

www.bukobasports.comMeneja Jurgen Klopp amelazimika kuziba ufa wa Difensi yake baada ya kuumia Martin Skrtel na Dejan Lovren na haraka akaingia Sokoni kumchukua Beki wa QPR, Steben Caulker, mwenye Miaka 24, ambae alikuwa Southampton kwa Mkopo.
Kwa vile Dili hii imekamilika Leo kabla ya Saa 6 Mchana, kwa Saa za Uingereza, basi Kanuni za huko zinamruhusu Jumatano kuichezea Liverpool itakaposhuka Uwanjani kwao Anfield kuivaa Arsenal ambao ndio Vinara wa Ligi Kuu England.
Leo Caulker ametarajiwa kufanya Mazoezi na wenzake wapy wa Liverpool.
Mbali ya Caulker, Liverpool pia wameimarika kwenye Difensi yao baada ya kuthibitika Majeruhi wao wengine, Kolo Toure na Mamadou Sakho, sasa wako fiti kuivaa Arsenal.