Thursday, January 28, 2016

UHAMISHO JANUARI: PATO ATUA STAMFORD BRIDGE, RAMIRES ATIMKIA CHINA KWENYE KLABU YA JIANGSU SUNING.

WAKATI Mbrazil wa Chelsea Ramires aking’oka kwenda kujiunga na Klabu ya China Jiangsu Suning kwa Dau la Milioni 25, Mbrazil mwingine Alexandro Pato ametua Stamford Bridge kukamilisha Dili ya Mkopo.
Ramires, Kiungo wa Miaka 28 ambae Msimu huu ameanza Mechi 7 tu za Ligi za Chelsea, alikamilisha Dili ya kuhamia China Mwezi Oktoba.

Klabu ya China Jiangsu Suning ipo chini ya Meneja Dan Petrescu ambae ni Mchezaji wa zamani wa Chelsea.
Akiwa na Chelsea, Ramires alicheza Mechi 251 na kufunga Bao 34 tangu ajiunge nayo Mwaka 2010 akitokea Benfica kwa Dau la Pauni Milioni 17.
Akiwa na Chelsea, Ramires alifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England, FA CUP, Kombe la Ligi, UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
WAKATI huo huo, Straika wa Brazil, Alexandre Pato, ametua Jijini London ili kukamilisha Dili ya kuhamia Chelsea kutoka Klabu ya Corinthians ya Brazil kwa Mkataba wa Mkopo wa Miezi 6 ambao unaweza kuwa wa kudumu mwishoni mwa Msimu.

Tayari Chelsea na Pato, mwenye Miaka 26, washaafikiana maslahi binafsi ya Mchezaji huyo.
Wakati akiingia London, Pato amesema ni ndoto kuhamia Stamford Bridge.
Pato