Saturday, January 23, 2016

UHAMISHO: MANCHESTER UNITED MBIONI KUMNASA KINDA WA BENFICA RENATO SANCHES

Renato SanchesManchester United wako mbioni kumsaini Kiungo kinda wa Klabu ya Ureno Benfica Renato Sanches.
Kijana huyo wa Miaka 18 anasifika sana huko Portugal na Mkataba wake una kipengele cha kutakiwa Dau la Pauni Milioni 60 ikiwa Klabu nyingine itataka kumnunua na kuvunja Mkataba wake wa sasa na Benfica.
Lakini inaaminika Benfica itakubali nusu ya Pesa hizo kutoka kwa Man United lakini Mchezaji huyo ambae pia huchezea Portugal U-21 atatakiwa kubaki huko Benfica hadi mwishoni mwa Msimu.
Inasemekana Man United walitaka kukamilisha Dili hii mwishoni mwa Msimu lakini wamelazimika kufanya biashara hivi sasa kutokana na Klabu nyingine kubwa kumwania kinda huyo.
Mchezaji huyo anafananishwa na Lejendari wa Brazil Ronaldinho kwa uwezo wake ambao humiliki Mpira vizuri sana na ana uwezo wa kucheza kama Kiungo Mshambuliaji na pia kama Winga.
Wasaka Vipaji wa Man United walimstukia Renato wakati walipoenda kumstadi Mchezaji mwingine wa Benfica, Goncalo Guedes.