Friday, January 22, 2016

UHAMISHO MWEZI JANUARI: LIVERPOOL KUMSAJILI ALEX TEIXEIRA ALIYEKUWA ANATAKWA NA CHELSEA PIA

Liverpool inamuandama mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira huku Jurgen Klopp akijaribu kufanya usajili wa kwanza tangu alipokuwa mkufunzi wa Anfield.
The Reds kama wanavyojiita wako tayari kulipa pauni milioni 24.5 kwa saini ya mchezaji huyo wa miaka 26.
Hatahivyo kilabu hiyo ya Ukraine inasema kuwa Texeira ambaye pia amehusishwa na uhamisho katika kilabu ya Chelsea atagharimu pauni milioni 39.
Klopp anapanga kuimarisha safu yake ya mashambulizi huku Danny Ings,Divock Origi na Daniel Sturridge wakiwa wanauguza majeraha.
Huku Christian Benteke aliyeighrimu kilabu hiyo pauni milioni 32 akisalia,Liverpool imefunga mabao 25 pekee katika mechi 22 za ligi msimu huu.

Shakhtar ambao wako katika mazoezi mjini Florida wanamthamini sana Texeira.
Amefunga mabao 22 katika mechi 15 na mabao manne katika mechi 10 za kilabu bingwa Ulaya simu huu.
Alianza kuchezea kilabu ya Vasco da Gama kabla ya kuelekea Shakhtar mwaka 2010.