Tuesday, January 26, 2016

VAN GAAL HAKUOMBA KUJIUZULU

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal hakuomba kujiuzulu wikendi iliopita, licha ya kuwa na madai hao.
Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 alidaiwa kumuomba naibu mwenyekiti wa kilabu hiyo Ed Woodward kwamba angejiuzulu kufuatia kushindwa kwa kilabu hiyo katika mechi ya ligi dhidi ya Southampton.
Duru zimearifu BBC michezo kwamba hakuna mazungumzo kama hayo yaliofanyika.
Van Gaal alirudi katika uwanja wa mazoezi wa kilabu hiyo siku ya jumanne huku wakijiandaa kwa mechi ya kombe la FA ya awamu ya nne dhidi ya Derby County siku ya ijumaa.