Sunday, January 10, 2016

WAKALA WA YAYA TOURE SELUK AHOFIA PEP GUARDIOLA KUTUA CITY!

www.bukobasports.comWAKALA wa Kiungo wa Manchester City Yaya Toure anahofia Klabu hiyo kumteua Pep Guardiola kuwa Meneja wao.
Huku mwenyewe akitangaza kuwa atafundisha Klabu ya Ligi Kuu England Msimu ujao baada ya kukataa kuongeza Mkataba na Klabu yake ya sasa Bayern Munich ambayo tayari imeshamchukua Carlo Ancelotti kumbadili yeye, Pep Guardiola anategemewa kutua City ingawa pia inadaiwa Klabu za Chelsea na Man United pia zinamwinda.
Ujio huo umemtia hofu Seluk, Wakala wa Yaya Toure mwenye Makao yake huko Monaco, ambae pia amemkandya Guardiola.
Seluk ameeleza: “Pep ni Kocha mzuri lakini ametwaa Mataji akiwa na Barcelona na Bayern. Ukweli ni kuwa hata Babu yangu angetwaa Mataji huko kwa sababu hizo ni Klabu kubwa na zina Wachezaji wazuri. Tizama Luis Enrique sasa. Msimu uliopita ametwaa Ubingwa wa La Liga na UEFA CHAMPIONS LIGI. Akiwa AS Roma hakufanya lolote. Nataka kuona Pep akiichukua Timu ya Nafasi ya 8 au 9 na kuwafanya Mabingwa!”
Hofu ya Seluk kuhusu Guardiola ni kutokana na Kocha huyo kumuuza Yaya Toure kwa Man City Mwaka 2010 walipokuwa wote Barcelona.
Seluk ameeleza: “Sijui mipango ya Guardiola lakini baada ya kile kilichotokea Barcelona inatia wasiwasi kwamba akienda City basi Yaya atakuwa nje.”
Pia Seluk ameeleza kuwa akiwa City, Guardiola atajaza Wachezaji wa kutoka kwao Spain na kutaka kuigeuza Klabu hiyo kuwa Barcelona nyingine.