Wednesday, January 20, 2016

YAYA TOURE MGUU NJE NDANI MAN CITY! WILFRIED BONY AKANA KUTAKA KUONDOKA!

KIUNGO wa Manchester City Yaya Touré anatafakari kuihama Klabu hiyo mwishoni mwa Msimu huu kwa mujibu wa Wakala wake, Dimitri Seluk.
Mkataba wa Toure, mwenye Miaka 32, na City unamalizika Mwakani Mwezi Juni na awali Mchezaji huyo wa Ivory Coast alisikika akisema atabaki City lakini Wiki hii zimeibuka Ripoti kuwa Klabu ya China, Shanghai SIPG, inataka kumsaini.
Seluk amekiri kuwa wao wapo tayari kusikiliza Ofa yeyote.
Akiongea na Jarida la SportItalia, Seluk alieleza: “Hatahama Januari. Lakini mwishoni mwa Msimu mambo yanaweza kubadilika. Tupo tayari kusikiliza Ofa yeyote ile.”
Wakati huo huo, Mchezaji mwenzake Toure wa City na Ivory Coast, Wilfried Bony, amekanusha uvumi kuwa anataka kuihama City.

Imedaiwa Bony anataka kurudi Klabu yake ya zamani Swansea City baada ya kumhoji Meneja Manuel Pellegrini kwanini hakumuanzisha kwenye Mechi na Arsenal Mwezi Desemba.