Saturday, February 13, 2016

FULL TIME: ARSENAL 2 v 1 LEICESTER CITY, DANNY WELBECK AITEKETEZA LEICESTER DAKIKA ZA MAJERUHI AKITOKEA BENCHI!


Arsenal Leo wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuwafunga Mtu 10 Leicester City Bao 2-1.
Ushindi huu umewafikisha Arsenal Pointi 51 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester na sasa wako Nafasi ya Pili lakini wanaweza kushushwa baadae Leo ikiwa Tottenham itaifunga Man City huko Etihad.

Jamie Vardy alifunga Penati ya Dakika ya 45 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kuangushwa na Monreal na kuipa Leicester Bao la kuongoza. Hadi Mapimziko, Arsenal 0 Leicester 1.
Kipindi cha Pili Dakika ya 54, Leicester walibaki Mtu 10 baada ya Simpson kupewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kumvuta Mkono Giroud na hivyo kuonyeshwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 70 Arsenal walisawazisha Bao kupitia Theo Walcott alieingia Dakika ya 60 kumbadili Coquelin.
Bao la ushindi kwa Arsenal lilifungwa na Danny Welbeck, Mchezaji ambae alikuwa Majeruhi tangu Aprili Mwaka Jana na kuingizwa Dakika ya 83 kumbadili Oxlade-Chamberlain, na kufunga Bao hilo muhimu katika Dakika ya 94 kwa Kichwa kufuatia Frikiki ya Mesut Ozil.
Danny Welbeck alitokea Benchi na kuipa ushindi Gunners kwa kufanya 2-1 katika dakika za lala salama ya 90.1-1Theo Walcott dakika ya 70 aliisawazishia bao Arsenal kwa kufanya 1-1 Danny Simpson (Leicester City) dakika ya 54  anaondoshwa kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano!1-0 Vardy akipongezwa kwa baoVardy ndiye aliyeifungia bao la kuongoza Leicester kipindi cha kwanza mwishoni kwa mkwaju wa penati dakika ya 45 na kwenda mapumziko Leicester wakiwa mbele ya bao 1-0.Cech bado anaendelea kuisaidia michomo Arsenal
VIKOSI:
Arsenal walioanza XI:
Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez, Giroud
Arsenal Akiba: Ospina, Walcott, Flamini, Chambers, Welbeck, Campbell, Elneny
Leicester City starting XI: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Drinkwater, Kante, Albrighton, Okazaki, Vardy
Leicester AkibaKing, Gray, Ulloa, Dyer, Wasilewski, Chilwell, Schwarzer
Vardy akipewa njia ya kufanya lolote kuleta mabadiliko Uwanjani