Wednesday, February 24, 2016

ARSENE WENGER ALIA NA WACHEZAJI WAKE KUTENDA MAKOSA YALE YALE!

Arsene Wenger ameponda kasoro za Timu yake Arsenal za kurudia makosa yao ya nyuma baada ya Jana kuchapwa 2-0 na Barcelona wakiwa Nyumbani kwao Emirates Jijini London katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL.
Bao zote hiyo Jana zilifungwa na Lionel Messi huku moja likiwa la Penati.
Katika Mechi hiyo, Arsenal walikosa nafasi kadhaa za kufunga na udhaifu wao kwenye Difensi, kama ule waliouonyesha Msimu uliopita walipotolewa na AS Monaco katika hatua hii hii ya Mashindano haya.

Baada ya Mechi, Wenger alidhirisha fedheha yake kwa maneno yake: “Inavunja moyo kuwapa Magoli tuliyowapa, hasa Bao la kwanza. Nadhani tuna hatia kubwa na hatuna kisingizio kwa Bao lile. Wao ni bora kupita sisi na kila Mtu anajua hilo lakini tungeweza kushinda Gemu kama tungekuwa na nidhamu ya uchezaji hadi mwisho! Kama ilivyokuwa na Monaco, kwa mara nyingine tumefungwa vile vile!”
Wenger aliongeza: “Tulipata nafasi 2 au 3 ya kulizuia Bao la kwanza lakini hatukufanya!”

Arsenal na Barca zitarudiana huko Nou Camp hapo Machi 16 na alipohojiwa kama atachezesha Kikosi dhaifu katika Mechi hiyo, Wenger alijibu: “Barcelona wameshafuzu kwa Asilimia 95 lakini tutaenda kule kucheza. Sisi ni Arsenal Football Club. Ni sisi na hatutaenda kule bila matumaini. Kushindwa kwetu ni kutotumia nafasi ya kuwafunga na nafasi ilikuwepo. Hilo ndio tunajutia. Mara nyingine unafungwa na Timu na huwezi kufanya lolote lakini hii ilikuwepo nafasi kuwafunga!”