Friday, February 26, 2016

BREAKING NEWS: GIANNI INFANTINO RAIS MPYA WA FIFA HADI 2019


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, sasa ndie mrithi wa Sepp Blatter baada ya kushinda Uchaguzi huko Zurich, Switzerland hii Leo.
Infantino aliwabwaga Wagombea wengine ambao ni Rais wa Shirikisho la Soka la Asia, Sheikh Salman, Jerome Champagne wa France na Prince Ali Bin Al Hussein wa Jordan.
Mgombea mwingine kutoka South African, Tokyo Sexwale, alijiengua kabla Kura hazijapigwa.
Katika Uchaguzi huo, Infantino alizoa Kura 88 na Salman 85 na kulazimisha kufanyika kwa Raundi ya Pili ya upigaji Kura kwa vile idadi inayotakiwa ya kuwa na Kura zaidi ya Theluthi 3 haikufikiwa ambayo Mshindi alitakiwa kuwa na Kura zaidi ya 104.

Katika Raundi ya Pili ya Kura, Infantino alizoa Kura 115 na sasa ndie Rais wa FIFA hadi 2019.

Raundi ya kwanza alikaribian kwa 88 na 85 na raundi ya pili akaibuka kwa 115 dhidi ya 88 Gianni Infantino