Saturday, February 13, 2016

CAF CHAMPIONS LIGI: YANGA YASHINDA BAO 1-0 VISIWANI MAURITIUS!

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo wameanza Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Cercle de Joachim ya Visiwa vya Mauritius kwa ushindi wa Bao 1-0.
Bao hili muhimu la Ugenini la Yanga lilifungwa na Straika Donald Ngoma katika Dakika ya 17.
Mara baada ya Mechi yao hiyo ya Mauritius, Yanga watarejea Nyumbani na kupiga Kambi huko Visiwani Pemba ili kujifua kwa ajili ya Mechi yao ya Februari 20, ile Dabi ya Kariakoo, dhidi ya Mahasimu wao Simba ikiwa ni Mechi ya Ligi Kuu Vodacom.

Yanga watarudiana na Cercle de Joachim hapo Tarehe 20 Februari Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

CAF CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Awali
Ratiba/Matokeo:
Ijumaa Februari 12

Vipers (Uga) 1 Enyimba (Nig) 0
Olympique Khouribga (Mar) 2 Gamtel (Gam) 1

Jumamosi Februari 13
Cercle De Joachim (Mau) 0 Young Africans (Tan) 1
Ashanti (Gha) v MO Bejaia (Alg)
C.R.D. Libolo (Ang) v Micomeseng (Gnq)
Centre Chiefs (Bot) v Ferroviario Maputo (Moz)
Chicken Inn (Zim) v Mamelodi Sundowns (Rsa)
Club Africain (Tun) v Tanda (Civ)
CotonTchad (Cha) v ASEC Mimosas (Civ)
Douanes (Sen) v Horoya (Gui)
Gor Mahia (Ken) v CNaPS Sport (Mad)
Lioli (Les) v Vital'O (Bur)
Mafunzo (Tan) v Vita Club (Drc)
Mangasport (Gab) v Etoile du Congo (Con)
Mbabane Swall. (Swa) v APR (Rwa)
Nimba (Lib)v Union Douala (Cmr)
Onze Createurs (Mli) v Al Ahly Tripoli (Lib)
St. Georges (Eth) v St Michel United (Sey)
Stade Malien (Mli) v Bobo-Dioulasso (Bur)
Volcan Club (Com)v Kaizer Chiefs (Rsa)
Warri (Nig) v Praia Cruz (Sao)


Wydad (Mar) v Douanes Niamey (Nig)
ZESCO (Zam) v Al-Ghazal (Ssu)

**Mechi za Marudiano Februari 27
**Washindi kuingia Raundi ya Kwanza ya Mtoano