Sunday, February 28, 2016

CHEKA AONYESHA CHECHE DAR, AMMALIZA MSERBIA KWA POINTI DAR

Bondia Mtanzania, Francis Cheka ameibuka na ushindi kwa kumpiga Geard Ajetovic kwa ushindi wa pointi huku majaji wote wakimpa ushindi. Sasa ndiye bingwa mpya wa mabara, ubingwa ambao aliupoteza kwa kupigwa nchini Russia mwaka 2014. Ajetovic raia wa Serbia anayeishi nchini Uingereza alipinga baada ya kudai ndiye alicheza vizuri zaidi. Katika pambano hilo kuwania ubingwa wa Mabara, Cheka alionekana kupiga ngumi nyingi za kudokoa lakini hazikuwa na nguvu sana kama za mpinzani wake aliyepiga ngumi chache lakini kali.