Friday, February 12, 2016

DIEGO COSTA AUMIA PUA JANA MAZOEZINI, WACHEZAJI CHIPUKIZI KUZIBA PENGO LAKE! AU KAMA VIPI ATAVAA MASK

Meneja wa Chelsea Guus Hiddink amefichua kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Diego Costa aliumia puani akishiriki mazoezi jana jioni.
Hata hivyo, Mholanzi huyo amesema Costa hayumo hatarini na anatarajiwa kufanya mazoezi madogo leo jioni na kisha kujiunga na wachezaji wenzake hotelini.
Costa anatarajiwa kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Newcastle.
Hiddink amesema Costa aliumia kimakosa akijaribu kupiga mpira wa kichwa.

Costa hujulikana sana kutokana na utukutu wake uwanjani.
Kuhusu beki wa Ufaransa Kurt Zouma, Hiddink amesema mchezaji huyo hataweza kucheza tena msimu huu baada ya kuumia kwenye goti wakati wa mechi dhidi ya Manchester United.
Hata hivyo, amesema klabu hiyo itatumia wachezaji chipukizi kuziba pengo atakaloacha.