Tuesday, February 2, 2016

DIRISHA LA UHAMISHO WA JANUARI WAFUNGWA RASMI!! DEBUCHY AONDOKA ARSENAL, POWELL NAE ACHOMOLEWA OLD TRAFFORD, NIASSE ATUA EVERTON KWA MBWEMBWE!!, DOUMBIA ATUA NEWCASTLE...

Dirisha lafungwa kiaina....Klabu kubwa zashindwa kununua Wachezaji kutokana na Bei kubwa za Wachezaji.
Newcastle waachia pesa £12million kumsaini Jonjo Shelvey kutoka  Swansea City tangu mapema mwezi uliopita

Mmiliki  Mike Ashley aliamua kuachia pesa
Newcastle United wanunua Winga matata Andros Townsend kutoka Tottenham kwa  £12million

Stoke waweka rekodi kwa kununua Mchezaji kwa  £18.3million wa  Giannelli Imbula kutoka Porto
Dirisha la Uhamisho la Januari 2016 limefungwa rasmi Saa 9 Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki.
Zifuatazo ndizo baadhi ya Dili zilizokamilika Dakika za mwisho kwa Ligi Kuu England.

OUMAR NIASSE ATUA EVERTON
Everton imemsaini Fowadi wa Senegal Oumar Niasse kutoka Klabu ya Urusi Lokomotiv Moscow kwa Dili ya Pauni Milioni 13.5
Niasse, mwenye Miaka 25, amefunga Bao 13 katika Mechi 23 za Lokomotiv Msimu huu na amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Nusu huko Everton.
Niasse anajiunga na Everton wakati Fowadi wao, Steven Naismith, akiondoka na kujiunga na Norwich na Winga Aiden McGeady akienda Sheffield Wednesday kwa Mkopo.

DEBUCHY AENDA BORDEAUX KWA MKOPO
Beki wa Arsenal Mathieu Debuchy amejiunga Klabu ya France inayocheza Ligue, Bordeaux, kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Debuchy alijiunga na Arsenal Julai 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 12 kutoka Newcastle.
Msimu huu, Debuchu, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa France, ameichezea Arsenal Mechi 7 tu na hajakanyaga Uwanjani tangu Novemba.

FLETCHER MKOPO MARSEILLE
Straika mkongwe wa Sunderland Steven Fletcher amejiunga na Klabu ya France Marseille kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Fletcher, mwenye Miaka 28 na ni Mchezaji wa Kimataifa wa Scotland, Msimu huu amefunga Bao 4 tu katika Mechi 18 alizoichezea Sunderland.
Fowadi huyo alijiunga na Sunderland Agosti 2012 akitokea Wolves kwa Dau la Pauni Milioni 14.

NICK POWELL WA MAN UNITED ATUA HULL CITY
Hull City imemsaini Mchezaji wa Manchester United Nick Powell kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Powell, mwenye Miaka 21, ameichezea Man United Mechi 2 tu Msimu huu.
Kijana huyo alianzia Soka lake huko Crewe na kujiunga na Man United Mwaka 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 3;

SEYDOU DOUMBIA ATUA NEWCASTLE
Newcastle imemsaini Fowadi wa AS Roma ya Italy ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Seydou Doumbia, kwa Mkopo.
Doumbia, mwenye Miaka 28, atakuwa Newcastle hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Doumbia alijiunga na AS Roma Januari 2015 lakini alicheza Mechi 13 tu na kisha Mwezi Agosti 2015 kurudi kwa Mkopo Klabu yake ya zamani CSKA Moscow.
LIGI KUU ENGLAND & LIGI KUU SCOTLAND:
-DILI ZA SIKU YA MWISHO-Februari 1:
Saa 23: 58 - John Souttar [Dundee Utd - Hearts] Ada Haikutajwa
23:15 - James Maddison [Coventry - Norwich] Ada Haikutajwa
22:45 - Marco van Ginkel [Chelsea - PSV] Mkopo
22:34 - Giannelli Imbula [Porto - Stoke] £18.3m
22:30 - Lee Hodson [MK Dons - Kilmarnock] Mkopo
22:30 - Yohan Benalouane [Leicester - Fiorentina] Mkopo
22:15 - Gary Dicker [Carlisle - Kilmarnock] Bure
22:02 - David Goodwillie [Aberdeen - Ross County] Mkopo
22:02 - Simon Church [MK Dons - Aberdeen] Mkopo
22:00 - Leroy Fer [QPR - Swansea] Mkopo
20:46 - Oumar Niasse [Lokomotiv Moscow - Everton] £13.5m
20:21 - Adalberto Penaranda [Udinese - Watford] Ada Haikutajwa
20:05 - Abiola Dauda [Vitesse Arnhem - Hearts] Mkopo
19:10 - Aidan Nesbitt [Celtic - Partick Thistle] Mkopo
19:06 - Colin Kazim-Richards [Feyenoord - Celtic] Ada Haikutajwa
18:34 - Abdoulaye Doucoure [Rennes - Watford] Ada Haikutajwa
18:10 - Rhoys Wiggins [Sheffield Wednesday - Bournemouth] Ada Haikutajwa
14:25 - Morgaro Gomis [Hearts - Motherwell] Mkopo
14:24 - Don Cowie [Wigan - Hearts] Bure
13:35 - Alex Pritchard [Tottenham - West Brom] Mkopo
13:26 - Patrick Roberts [Manchester City - Celtic] Mkopo
11:12 - Seydou Doumbia [Roma - Newcastle] Mkopo
09:07 - Antonio German [Kerala Blasters - Partick Thistle] Bure
Wengine:
23:15 - James Maddison [Norwich - Coventry] Mkopo
23:00 - Dominic Vose [Wrexham - Scunthorpe] Ada Haikutajwa
22:46 - Baily Cargill [Bournemouth - Coventry] Mkopo
22:30 - Nikolay Bodurov [Fulham - FC Midtjylland] Mkopo
22:23 - Julien De Sart [Standard Liege - Middlesbrough] Ada Haikutajwa
22:21 - Jay Emmanuel-Thomas [QPR - MK Dons] Mkopo
22:21 - Alex Revell [Cardiff - MK Dons] Bure
22:20 - Jordi Gomez [Sunderland - Blackburn] Mkopo
22:20 - Shane O'Neill [Apollon Limassol - Cambridge] Mkopo
22:15 - James Baxendale [Walsall - Mansfield] Bure
22:15 - Sacha Petshi [Blackburn - US Creteil-Lusitanos] Ada Haikutajwa
22:00 - Shaun Tuton [Halifax - Barnsley] Ada Haikutajwa
21:40 - Jamie Proctor [Fleetwood - Bradford] Bure
21:34 - Ritchie de Laet [Leicester - Middlesbrough] Mkopo
21:31 - Jack Stephens [Southampton - Coventry] Mkopo
21:31 - Nick Powell [Manchester United - Hull] Mkopo
21:27 - Rod Fanni [Al-Arabi SC - Charlton] Mkopo
21:19 - Conor McAleny [Everton - Wigan] Mkopo
21:16 - Dusan Kuciak [Legia Warsaw - Hull] Ada Haikutajwa
21:00 - Steven Fletcher [Sunderland - Marseille] Mkopo
21:00 - Yaya Sanogo [Arsenal - Charlton] Mkopo
20:45 - Jordan Rhodes [Blackburn - Middlesbrough] £9m
20:36 - Ryan Hedges [Swansea - Stevenage] Mkopo
20:30 - Mathieu Debuchy [Arsenal - Bordeaux] Mkopo
20:30 - Jerome Binnom-Williams [Crystal Palace - Leyton Orient] Mkopo
20:30 - Jiri Skalak [FK Mlada Boleslav - Brighton] Ada Haikutajwa
20:26 - Francesco Pisano [Bolton - U.S. Avellino 1912] Mkopo
20:07 - Dominic Hyam [Reading - Dagenham] Mkopo
20:00 - Danny Rose [Oxford - Northampton] Bure
19:53 - Charlie Harris [Brighton - Barnsley] Ada Haikutajwa
19:30 - Tom Anderson [Burnley - Chesterfield] Mkopo
19:20 - Michael Smith [Swindon - Portsmouth] Mkopo
19:00 - Paul Jones [Portsmouth - Crawley] Mkopo
18:35 - Josh Laurent [Brentford - Hartlepool] Bure
18:15 - James Tarkowski [Brentford - Burnley] Ada Haikutajwa
18:00 - Ryan Allsop [Bournemouth - Wycombe] Mkopo
18:00 - Zakaria Labyad [Sporting Lisbon - Fulham] Mkopo
17:59 - Gary MacKenzie [Doncaster - Notts County] Mkopo
17:31 - Nadir Ciftci [Celtic - Eskisehirspor] Mkopo
17:30 - Daniel Alfei [Swansea - Mansfield] Mkopo
17:30 - Gary Liddle [Bradford - Chesterfield] Ada Haikutajwa
17:30 - Elvis Manu [Brighton - Huddersfield] Mkopo
17:00 - Abdenasser El Khayati [Burton - QPR] Ada Haikutajwa
16:57 - Michael O'Halloran [St Johnstone - Rangers] Ada Haikutajwa
16:49 - Eder [Swansea - Lille] Mkopo
16:40 - Pat Hoban [Oxford - Stevenage] Mkopo
16:13 - Connor Dimaio [Sheffield United - Chesterfield] Bure
15:44 - Zeli Ismail [Wolves - Oxford] Mkopo
15:31 - Aaron O'Connor [Forest Green - Stevenage] Ada Haikutajwa
15:30 - Louis Thompson [Norwich - Swindon] Mkopo
15:00 - Kelle Roos [Derby - AFC Wimbledon] Mkopo
14:31 - Nicky Hunt [Mansfield - Leyton Orient] Ada Haikutajwa
14:25 - Chris Maguire [Rotherham - Oxford] Bure
13:00 - Tom Nichols [Exeter - Peterborough] Ada Haikutajwa
13:00 - Rohan Ince [Brighton - Fulham] Mkopo
12:59 - Aiden McGeady [Everton - Sheffield Wednesday] Mkopo
12:46 - Kevin van Veen [Scunthorpe - SC Cambuur Leeuwarden] Mkopo
12:00 - Richard O'Donnell [Wigan - Bristol City] Ada Haikutajwa
12:00 - Tom Lawrence [Leicester - Cardiff] Mkopo
11:34 - Chris Neal [Port Vale - Doncaster] Mkopo
11:30 - Luke James [Peterborough - Hartlepool] Mkopo
10:01 - Kenneth Zohore [KV Kortrijk - Cardiff] Mkopo
Dili zilizokamilika kabla:
31 January
Emmanuel Emenike [Fenerbahce - West Ham] Mkopo
Alex Jones [Birmingham - Wellington Phoenix] Mkopo
Florian Thauvin [Newcastle - Marseille] Mkopo