Monday, February 22, 2016

EMIRATES FA CUP: LEO NI MAN UNITED vs SHREWSBURY TOWN, WAKISHINDA KUIKABIRI WEST HAM UNITED OLD TRAFFORD ROBO FAINALI!

LEO Manchester United wako Ugenini kucheza na Timu ya Daraja la chini la Ligi 1, Shrewbury Town, katika Mechi ya mwisho ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP ambayo Mshindi wake atakuwa Nyumbani kucheza na West Ham kwenye Raundi ya 6 ambayo ni Robo Fainali.
DROO ya kupanga Mechi za Raundi ya 6 ambazo ndio Robo Fainali ya Kombe Kongwe Duniani, FA CUP, ambalo sasa linaitwa EMIRATES FA CUP baada ya udhamini wa Kampuni ya Ndege ya UAE, Emirates Airlines, ilifanyika Jana huko Stamford Bridge mara baada ya Chelsea kuitwanga Man City 5-1 kwenye Mechi ya Raundi ya 5 ya Kombe hili.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Manchester United kukutana na Shrewsbury Town
Ambao kwa sasa wanasuasua kwenye Ligi 1 wakiwa Nafasi ya 19 ikiwa ni Pointi 3 tu juu ya Timu zile ziko hatarini kushuka Daraja.
Lakini nao Man United wanatinga kwenye Mechi hii kutoka kwenye vichapo viwili mfululizo toka kwa Sunderland kwenye Ligi Kuu England na FC Midtjylland kwenye EUROPA LIGI.

Kwa Mwaka huu 2016, Man United, chini ya Meneja anaesakamwa Louis van Gaal, wameshinda Mechi 5, Sare 2 na kufungwa 3 katika Mechi zao 10 zikiwemo ushindi kwenye Raundi zilizopita za FA CUP dhidi ya Sheffield United na Derby County.

Shrewsbury wao wanatinga kwenye Mechi hii wakitika ushindi wa 3-2 walipocheza na Blackpool kwenye Ligi na kwenye Raundi zilizopita za FA CUP walizitoa Cardiff City na Sheffield Wednesday.
MAN UNITED vs SHREWSBURY TOWN